BODI YA LIGI YAIONYA YANGA SPORTS CLUB

MTENDAJI Mkuu wa bodi ya ligi Tanzania (TPLB) Almas Kasongo ameionya Yanga kuhusu kauli ya kutopeleka timu uwanjani na kusema kwamba kanuni zinataka kuishusha madaraja mawili timu itakayofanya kitendo hicho.




Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu, mechi ya kiporo ya Simba na Yanga imepangwa kuchezwa Julai 3 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam baada ya ile ya Mei 8 kushindikana.

Mechi hiyo awali ilipangwa

kuchezwa Mei 8 lakini haikufanyika baada ya kutokea sintofahamu kutokana na serikali kuagizwa isogezwe mbele kutoka saa 11 jioni mpaka saa moja usiku.

Msemaji wa Yanga Hassan Bumbuli juzi alinukuliwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwamba hawautambui mchezo huo kwani wao walishamaliza tangu Mei 8.

Kasongo alisema jana kanuni ziko wazi kuhusu timu itayoshindwa kutokea uwanjani ikiwa ni pamoja na kushushwa madaraja mawili.

“Usipopeleka timu uwanjani timu husika inashuka madaraja mawili, bado sijajua msingi wa kauli ya huyo mtu ni nini, niwakumbushe viongozi wa soka kabla hujazungumza uzifikirie kanuni zinasemaje,” alisema.

Alisema viongozi wawe makini kutamka maneno kuhusu jambo ili wasiende kinyume na taratibu zilizopo.

Hata hivyo, kauli aliyotoa Bumbuli inakinzana na ile aliyotoa Kaimu Katibu wa Klabu hiyo Haji Mfikirwa aliyesema sio tamko la klabu na kwamba wao watatoa msimamo juu ya mchezo huo.

Mwenyekiti wa TPLB Steven Mguto alisema kama kweli klabu hiyo haitafanya ilichotamka basi ingetumia njia sahihi kwa kuandika barua lakini sio kama ambavyo amefanya msemaji huyo

Like page
Sega Sports✓

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii