De BRUYNE HATAHATI EURO 202


 KEVIN De Bruyne huenda akakosa mechi ya ufunguzi ya Ubelgiji kwenye michuano ya Euro 2020 dhidi ya Urusi Juni 12, amesema Roberto Martinez.

De Bruyne ni majeruhi baada ya kuumia usoni katika harakati za kuwania mpira dhidi ya beki wa Chelsea Antonio Rudiger kwenye mechi ya fainali za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester City mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kiungo huyo hajatakiwa kufanyiwa upasuaji lakini Martinez hana hakika kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atakuwa tayari.

Kama De Bruyne hatorejea uwanjani, bosi wa Ubelgiji amethibitisha atavaa mask kama inayovaliwa na Jan Vertonghen baada ya kuumia akiichezea Tottenham miaka miwili iliyopita.

Kevin De Bruyne alivunjika pua na kupata hitilafu kwenye jicho.

Akizungumza mapema wiki hii, bosi wa Ubelgiji Martinez alisema De Bruyne ahitaji upasuaji.

"De Bruyne anaonekana atakuwa fiti kwa mechi ya kwanza na kama atakuwa na mbadala nitasema.”

"Tumefanya maamuzi kuhusu mask yake, itakuwa kama ile ya Jan Vertonghen.”

"Nitasema wiki ijayo, hatujui kwa hakika tutakuwa vipi na Kevin kwa sasa muacheni apumzike.”

Ubelgiji itaanza kampeni za Euro 2020 dhidi ya Urusi kwenye uwanja wa St Petersburg Jumamosi ijayo.

Miamba hiyo namba moja kwenye ubora wa viwango vya Fifa, watakutana na Denmark Juni 17 kabla ya kucheza na Finland kwenye mechi ya mwisho ya kundi B Juni 21.

Like page✓
Sega Sports

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii